Miaka 60 ya uhuru:Kinamama wengine hawakujua kusoma -Mama Maria Nyerere

Iliyochapishwa

'Katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, ambayo sasa ni Tanzania, BBC imefanya mahojiano na watu mbalimbali, na miongoni mwao ni Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa baba wa Taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam, kwanza amemuulizia anajisikiaje kuona nchi inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru?