HIV: ‘Nililala stoo kutokana na hali yangu ya kiafya'

Iliyochapishwa

Msichana mwenye umri wa miaka 19 Veronica kutoka nchini Tanzania anaishi na virusi vya HIV na anaelezea changamoto alizokumbana nazo tangu alipogunduliwa ana virusi vya ukimwi akiwa na miaka mitano alipopatwa na ugonjwa wa ngozi.

Safari ya maisha yake haijawa rahisi lakini ameamua kuwahamasisha wengine wanaoishi na hali hiyo.

Je, ni mipango gani inayohitajika ili kupunguza unyanyapaa miongoni mwa wanaoishi na virusi vya ukimwi?