Zanzibar kukodisha visiwa vidogo kukuza utalii

Iliyochapishwa

Serikali ya Zanzibar imetangaza mpango wa kuanza kukodisha visiwa vidogo kwa lengo la kukuza utalii.

Visiwa hivyo vitakua na wamiliki binafsi huku vikifanyiwa ujenzi mkubwa kwa lengo la kuvutia watalii.

Licha ya kuwepo kwa maoni tofauti juu ya hatua hii, serikali ya Zanzibar inasisitiza kwamba hakuna madhara kwa wenyeji wa maeneo husika na kwamba ndio wanufaika wakubwa wa mpango huo.