Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Diamond Platnumz: 'Mafunzo muhimu niliyopata wakati wa janga la corona'
Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Diamond Platnumz Ijumaa hii amezindua kampuni ya kamari ya WasafiBet, katika hatua ambayo inalenga kuleta mseto wa mapato ya msanii huyo kando na muziki wake, mapato kutoka kwa matangazo ya bidhaa za kampuni mbali mbali na uwekezaji kwenye vyombo vya habari vya Wasafi radio na televisheni.
Katika mahojiano haya ya awali na mwanahabari wa kitengo cha BBC Biashara Hamida Abubakar, Diamond ameangazia mafunzo muhimu aliyopata wakati wa janga la corona pamoja na matarajio yake kuhusu msimu wa sherehe wa Disemba mwaka huu.