Serikali na wadau kushirikiana kuwezesha umri wa kuolewa uanzie miaka 18

Kabudi
Iliyochapishwa

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi amesema Serikali imepanga kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Rufani kwa kuandaa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kuhusu umri wa kuolewa, limeripoti gazeti la Mwananchi nchini humo.

Muswada huo anasema umepelekwa kamati ya Bunge kwa ajili ya kuupitia lakini iliurejesha serikalini ikitaka kuendelea kwa mashauriano na wadau.

Alisema wanaendelea kuwashirikisha wadau wengine kuona namna nzuri ya kutekeleza mahitaji ya watu ya umri wa kuolewa uwe kuanzia miaka 18.

''Mwaka 71 mwisho wa elimu ulikuwa ni darasa la saba kabla ya hapo darasa la nne. Kwa hiyo mabadiliko yametokea kwamba lazima tuiangalie sheria ya ndoa katika vipengele vingine''.

Profesa ameisema sheria hiyo ni ya kimapinduzi kwani imewezesha wanandoa kuweza kufanya kazi katika maeneo tofauti.

" Haya yalikuwa na sababu, mwaka wa 1971 ambazo kwa sasa huenda zisiwe sababu kwasababu, wakati huo mtoto wa miaka 16 alikuwa keshamaliza masomo katika darasa la saba na haendelei na masomo yake...awali walikuwa na wamaliza masomo yao katika darasa la nne.'' aliendelea kueleza waziri huyo.

Aliongeza kuwa ''Serikali ilitekeleza maagizo ya mahakama ya rufani na ikapeleka rasimu ya muswada bungeni ufikiriwe, lakini baada ya kamati bunge kuupitia, iliurejeshea serikali ikitaka iendelea na mashauriano na wadau mbalimbali. Kwa hivyo hivi sasa serikali inaendelea na mashauriano na wadau mbalimbali viongozi wa kidini ili baadaye tuone, umri wa mtoto wa kike kuolewa uwe ni miaka 18'' Alisema Prof Kabudi.

''Katiba inasema umri wa mtoto kuolewa ni miaka 18. Ambacho tunagombea hapa ni zile exceptions zilizotolewa. Anaweza kuolewa na umri huu kwa idhini ya wazazi ama anaweza kuolewa na umri chini ya miaka 18 kwa idhini ya mahakama .''

'Zamani usingefanya kazi mahali pengine ungekuwa umevunja ndoa'

Profesa Kabudi alisema hayo Novemba 18,2021 alipoeleza mafanikio ya wizara yake katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Kuhusu uwakilishi wa mawakili, Profesa Kabudi alisema mahakama zote za mwanzo zenye mahakimu wenye shahada ya sheria mawakili wanaruhusiwa katika mashauri yao.

Alisema ndani ya mwaka mmoja mahakama za mwanzo zote nchini zitakuwa na mahakimu wenye shahada ili mawakili waweze kutumika.

Kuhusu kutafsiri sheria ziwe kwa Kiswahili, Profesa Kabudi alisema hadi sasa Sheria 154 zimetafsiriwa katika rasimu ya awali na mchakatochuo unaendelea kwa miaka miwili.

"Tunatumia rasimu ya kwanza ili sheria hizi zitumike baada ya hapo tukibaini maeneo yanayohitaji marekebisho tutafanya. Jambo kubwa ni kuwa na istilahi za kisheria kwa lugha ya Kiswahili," alisema.

Mwanamke

Maandamano mikutano

Hakuna jambo linalofanyika bila utaratibu. Tunasoma sura ya pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuhusu haki za binadamu bila kusoma ibara ya 30 iliyoweka mipaka ya wewe kufaidi uhuru wako," alisema

Alipoulizwa kuhusu utaratibu wa makubaliano ya awali (plea bargain) unachochea watu kufanya makosa, Profesa Kabudi alisema Tanzania si nchi ya kwanza kuuanzisha na umekuwa ukitumika kwa miaka mingi Marekani na Uingereza. Alisema makubaliano hayo yana viwango, kanuni na utaratibu wake.

Kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa nchini Tanzania kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa kibali cha mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti, Raia Tanzania wanaheshimu sheria kuhusu ndoa za watoto?