COP26: Mpiga picha wa Tanzania ashinda tuzo
Wakati dunia ikiwa katika harakati za kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi, wapiga picha za matukio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi wameonekana kuwa ni moja ya vyanzo muhimu vya uelewa juu hasa maeneo yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi.
Mpiga picha wa Tanzania @imaninsamila ni mmoja wa waliobahatika kupata tuzo za vijana za EU GCCA+ tuzo ambayo inalenga kuwasaidia wanahabari wachanga, waandishi na wapiga picha kusambaza taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi kote ulimwenguni
Global Climate Change Alliance Plus ni mpango mkuu wa nchi za Ulaya (EU) ambao unasaidia nchi zilizo hatarini zaidi kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi hivyo kwa ushindi huu Nsamila amefurahi sana.
Mwandishi wa BBC@frankmavura alikutana na Imani Nsamila na kutueleza yale yaliyomfanya akatangazwa mshindi huko Brassels Ubelgiji na kutupa muelekeo wake baada ya tuzu hii.
#cop26 #EU #ClimateChange #GCCA+