Mtindo wa kufanya mazoezi kwa kusafisha mazingira wapata umaarufu Nigeria
Iliyochapishwa
Mtindo wa kusafisha mazingira wakiwa wanafanya mazoezi umepata umaarufu mkubwa kwa vijana wa nchini Nigeria.
Mtindo huu unaofahamika kama Plogging, ulianzia Sweeden mnamo mwaka 2016 na kuanza kupata umaarufu katika maeneo mengine ya dunia.
Mwanafunzi wa chuo kikuu ,Adeyemi Joy anatueleza jinsi mtindo huu ulivyobadilisha maisha yake.