Serikali iliingia madarakani katika kipindi kigumu sana kiuchumi-Dkt Mwinyi

Maelezo ya video, Serikali iliingia madarakani katika kipindi kigumu sana kiuchumi-Dkt Mwinyi
Iliyochapishwa

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dokta Hussein mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na Covid 19.

Katika hotuba ya maadhimisho ya mwaka mmoja utawala yake kwa taifa Rais Mwinyi amesema wakati anaingia madarakani ulikuwa wakati mgumu kutokana na kuyumba kwa uchumi kote duniani ikifahamika Zanzibar inategemea kwa kiasi kikubwa mapato kutoka kwenye sekta ya utalii.

Rais Mwinyi amesema ili kujinasua na mdororo huo wa kiuchumi wamepata mkopo mkubwa toka IMF ambao watautumia kulipa madeni mbali mbali ikiwemo ya wafanyakazi, ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo na huduma za kijamii kama vile hospitali kubwa katika kila mkoa na kwa ngazi ya wilaya.

Mwinyi pia ameendelea kuhimiza uwajibikaji na matumizi mazuri ya fedha ambazo zimeelekezwa kwenye miradi mbalimbali.

Rais Mwinyi na serikali yake ya awamu ya nane wamejipambanua kwa sera ya uchumi wa buluu ambayo kwa mujibu wa watendaji wake na wananchi tayari imeanza kulipa.

Maadhimisho haya ya mwaka mmoja yamefikia kilele baada ya shughuli za juma zima.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais mstaafu wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, na Maraisi wastaafu wa serikali ya mapindizi ya Zanzibar.

Kabla ya halfa ya hitimisho mapema asubuhi kulikuwa na mbio zilizopewa jina la uchumi wa buluu lengo likiwa ni kuonesha nia ya Serikali ya awamu ya nane kukuza michezo.