La Palma: 'Bomu la Lava lashuhudiwa likishuka mlimani kwa kasi kufuatia mlipuko wa volkano wa Cumbre Vieja

Iliyochapishwa

.Tazama video ya mpira wa jiwe lililoyeyuka linalojulikana kama 'Bomu la Lava' likibingirika chini ya mlipuko wa Volkano kutoka kwa mlima Cumbre Vieja katika kisiwa cha Uhispania cha La Palma.

Mlima huo umekuwa ukilipuka tangu mwezi Septemba. Milipuko yake imelazimu maelfu ya watu kuondoka katika nyumba zao na kuharibu majumba na mashamba.