Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bernard Membe: Niliumizwa sana, nilidhalilishwa sana
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya shilingi bilioni 6 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo.
Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.
Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.
Bernard Membe amezungumza na Martha Saranga akieleza namna alivyopokea uamuzi huo wa mahakama