Kulungu anasuliwa gurudumu lililokuwa shingoni mwake kwa miaka miwili

Iliyochapishwa

Maafisa wa wanyamapori huko Colorado wametumia zaidi ya miaka miwili kujaribu kuwa karibu na kulungu ambaye alinaswa gurudumu kwenye shingo yake.

Ripoti zilionekana kwa mara ya kwanza kuhusu kulungu huyo mnamo Julai 2019 baada ya kuonekana akizunguka na kifaa chake kipya.

Hata hivyo, ilikuwa vigumu sana na alikwepa kukamatwa hadi sasa hadi ulipofika wakati wa kupandwa kwa majike wakati wa msimu wa kujamiiana.