Familia yauza mtoto kwa dola 500 kuepuka njaa

Maelezo ya video, Familia yauza mtoto kwa dola 500 kuepuka njaa
Iliyochapishwa

Afghanistan inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani, huku nchi hiyo ikishuhudia kuzorota kwa kasi kwa hali nchini humo tangu wapiganaji wa Taliban wachukue mamlaka mwezi Agosti.

Fedha za msaada kutoka mataifa ya kigeni ambazo zilitegemeza uchumi duni wa nchi hiyo zimesimamishwa huku ulimwengu ukijadili jinsi ya kukabiliana na utawala wa Taliban.

Umoja wa Mataifa umetoa onyo kali - kwamba mamilioni ya watu watakufa ikiwa misaada ya haraka haitafika nchini humo hivi karibuni.

Katika video hii, mwandishi wa BBC Yogita Limaye anasafiri hadi Herat, magharibi mwa Afghanistan, na kujionea hali mbaya . Imetolewa na Imogen Anderson Imetayarishwa na kuhaririwa na Sanjay Ganguly