Mauaji ya Kimbari Rwanda: Jinsi mafunzo ya sanaa yanavyowaponya wajane wa mauaji hayo
Iliyochapishwa
Wajane wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wamekuwa wakipokea mafunzo ya sanaa ya michezo ya kijihami ikiwemo mchezo wa yoga kama njia ya kupona kutokana na majeraha waliyo nayo kwa miaka mingi kufuatia kupoteza wapendwa wao katika mauaji hayo.
Chini ya mradi uliopewa jina la ‘’ Martial Arts for justice’’ au michezo ya kujihami kwa ajili ya haki , ulioanzishwa na Master Dean raia wa Canada anayeshikilia mkanda mweusi katika Taekwondo,wakufunzi wenyeji hutoa mafunzo ya michezo ya kujihami ikiwemo Yoga kwa wanawake walio na umri zaidi ya 60 kama tiba ya kuponya vidonda visivyoonekana. Waliomaliza mafunzo hayo wanasema yaliwasaidia sana kimwili na kiakili.