Fahamu jinsi mlo wa miguu ya kuku unavyopendwa na Watanzania

Maelezo ya video, Fahamu jinsi mlo wa miguu ya kuku unavyopendwa na Watanzania
Iliyochapishwa

Biashara ya miguu ya kuku imezidi kushika kasi hasa ukizingatia ni Chakula kinachopendwa sana na familia nyingi nchini Tanzania.

Wapo wanaodhani si salama kutokana na chakula hiki kuuzwa zaidi maeneo ya mitaani na pembezoni mwa Barabara, lakini hiyo ni tofauti kwa wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wao hupendelea kula chakula hiki nyakati za jioni.

Mwandishi wa BBC Frank Mavura ametembea moja ya mitaa maarufu kwa uuzaji wa miguu ya kuku na utumbo jijini Dar es Salaam na kutuletea taarifa hii.