Ubunifu wa mvulana wa miaka 14 ulivyomsaidia kukabiliana na hali ngumu ya maisha

Chanzo cha picha, Cortesía de Carla Cabrera
Ana umri wa miaka 14 tu, lakini ujuzi wake umewashangaza wengi. Kwa mikono yake anaonekana kama mshonaji wa viatu , 'cholas', kama wanavyoitwa nchini Venezuela, akitumia taili na vitambaa.
Upande wa chini au soli ya kandambili hutumia magurudumu ya magari. Kwanza analitengeneza vizuri mithili ya nyayo, kisha anashonelea nguo kwenye kandambili za mchuchumio kwa ajili ya wateja wanawake . Ni kazi ngumu.
"Kuna watu hapa katika Ciudad Bolívar, ambao tayari wamekwisha fika mbali kimafanikio. Lakini walikuwa wafisadi, " anasema, huku akionekana kuridhika na kazi yake.
Ciudad Bolívar ni mji mkuu wa jimbo la Bolívar, lililoko kusini mashariki mwa Venezuella. Sawa na maeneo mengine ya nchi hiyo, mji huo unakabiliwa na mfumuka mkubwa wa bei , ukosefu wa upatikanaji dola , sarafu pekee ambayo inaweza kumruhusu mtu kuishi, na kumudu viwango vya juu vya bei za bidhaa za msingi.
Ni kutokana na hali hii ndipo mvulana López, alipobuni biashara ili kuisaidia familia yake kukabiliana na maisha magumu ya kila siku katika taifa hilo la Amerika Kusini.

Chanzo cha picha, Cortesía de Carla Cabrera
Kupotea kulikogeuka kuwa biashara
Wazo lilimjia usiku .Andrés López alipoteza kandambili zake na hakukuwa na pesa ya kukunua mpya.
Anaishi na mama yake, kaka yake mwenye umri wa miaka 17, na babu yake. Mama yake Carla Cabrera hawezi kufanya kazi kwasababu anaumwa ugonjwa wa kukosa damu mwilini na hivyo lazima akae nyumba.
"Kwahiyo nilichukua gurudumu nikajitengenezea kandambili mwenyewe. Zilionekana nzuri na nikahisi ninaweza kuziuza ," anasema mvulana huyo mwenye umri wa kubalehe.
"Kutokana na ugonjwa wangu, mvulana alihamasika kuuza cholas, " anasema mama yake.
Uamuzi wake ulitokana na matatizo ya familia katika kupata dola taslimu na kununua chakula.
Ubunifu na ujuzi aliurithi kwa babu yake Andrés , sonara Mhispania ambaye kalikuwa na karakana yake kando na nyumba yake.
Babu na mjukuu wake walitumia muda mwingi kuwa pamoja na hivyo Andrés alijifunza kutumia mikono yake .
López alikuwa akikusanya magurudumu katika eneo la karibu na nyumbani kwao , lakini hivi karibuni yameadimika na sasa analazimika kuyanunua au kutoa cholas kwa watu ili apewe gurudumu.
"Unahitaji soli na kuingiza uzi ndani ya kipande cha gurudumu. Sindano nyuma ya visigino vya wanawake. Huwa ninaichukua, ninaipaka rangi ya viatu na kuipatia muundo wa mguu ," anaeleza.

Chanzo cha picha, Cortesía de Carla Cabrera
Ukosefu wa dola na viwango vya chini vya maisha ya watu ni vya hali ya juu katika Venezuela kiasi kwamba wakati mwingine anasema hakuweza kupokea pesa za malipo ya kanda mbili zlizoziuza.
Wakati mwingine hulazimika kubadilisha kanda mbili kwa bidhaa za chakula ili walau kupata faida ya kazi yake, baada ya wateja ushindwa kumlipa.
"Alibadilisha kandambili kwa unga au vyakula vingine, ingawa nilisisitiza kuwa kila mara awe anajaribu kuwauzi ili walau aweze kujinunulia kitu fulani ," anasema mama yake Cabrera.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe, 1
Familia haikuwahi kufikiria kuwa kuuza cholas kunaweza kuwa chanzo chao kikuu cha mapato na hata kandambili hizo kuwa marufu kwenye mitandao.
Usaidizi
"Kwa sasa ninatengeneza cholas kwa oda. Watu hunipa kipimo chao cha mguu wanachotaka na rangi ambayo wangeipenda halafu nawatengenezea. Huwa ninatengeneza pea moja na kuuza kwa dola tano au sita , "anasema mvulana huyo.
Mauzo yalianza taratibu.
Cabrera anakiri kuwa kandambili ya kwanza aliyoitengeneza mtoto wake haikuwa nzuri sana : "Ujuzi wake umekuwa bora siku hadi siku."
Ndio maana anashuku kwa Imani na ushirikiano wa majirani, ambao tangu mwanzo walimuamini mbvulana wake na kumpatia kazi jambo lililomsaidia kuanzisha biashara.

Chanzo cha picha, Cortesía de Carla Cabrera
"Sasa inafurahisha, kwasababu tunapoketi nje ya nyumba yetu tunamuona karibu kila mtu amevaa kandambili za Andrés's cholas," anasema mama yake.
"Katika eneo letu kuna watu wanaougua kuvu na magonjwa mengine ya ngozi miguuni. Matatizo haya hayawapati wanapovaa kandambili ninazo watengenezea.
Mbali na hayo hazitelezi ," anaelezea Andrés kuhusu bidhaa yake.
Mama na mvulana wake wanaiona biashara yao kama mafanikio, ingawa katika Venezuela hii kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mafanikio.
Faida hutumiwa kwa matumizi ya chakula, garama za kutengeneza kandambili.
Kwahiyo, kwao kufahamika katika mitandao ya kijamii ni muhimu sana, ambapo mara kadhaa watu maarufu na washawishi wamekuwa wakihusika kutangaza kazi yake.
Pia msaada
Andrés López pia hutumia ujuzi wake katika kuendeleza huduma za kazi zamsaada.
Yeye pamoja na mama yake wanafuatilia kwa karibu kazi ya daktarin Mvenezuela María Torrealba kwenye Instagram, ambako anafanya kazi yake kama daktarin bingwa wa watoto wa umma.
Katka akaunti yake ya mtandao hushirikisha umma ugumu wa familia za Wavenezuela wa kupata dawa kwa ajili ya watoto wao. Huwa ninaandaa kampeni za kutafuta usaidizi kwa ajili yao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe, 2
Andrés walikuwa na wazo la kumuandikia daktari na kumpatia kandambili kama msaada kwa watoto wasiojiweza.
Watu wengi walishangaa wakati Torrealba alipotangaza wazi kutoa msaafda huo kwenye utambulisho wake wa Insrtagram. Hii ilimpatia umaarufu sana mvulana huyu katika kazi yake.
"Mara moja wattu wengi kutoka nje ya eneo, waliandika na kuagiza viatu na kusaidia. Mlimbwende wa zamani wa Venezuela, Daniela De Giacomo, alilipia viatu 30 ambavyo tulimpa Dkt Torrealba katika siku ya watoto kuvifikisha katika jamii ," anasema mama yake Andrés.
Hivi karibuni familia ilitoa kandambili 15 kwa majirani zao.
Mtu aliyeagiza na kuzinunua alimwambia Andrés azipeleke kwa yeyote aliyetaka kumpatia. Alizigawa kwa watoto na wzee katika jamii ambao walizihitaji
Mipango ya baadaye

Chanzo cha picha, Cortesía de Carla Cabrera
Carla Cabrera ana hofu kwamba mtoto wake atachukua majukumu ya familia
Hatahivyo, Andrés anaimani kuwa siku zijazo ataanzisha kampuni, awe na mahali pake pa kufanyia kazi na vifaa bora vya kutengenezea kandambili zake.
Eneo lililopo karibu na nyumbani kwao ambako babu yake alikuwa na karakana yake, liliungua na akabaki bila makazi. Moto ulilipua gesi na nyumba ikaungua, na kuangamia.
Wakati huo huo akaunti ya Instagram ya Andrés ina wafuasi wapatao 11,000 na biashara imepanuka hadi nje ya Bolívar , ambapo sasa anauza katika miji ya Caracas, Valencia na maeneo mengine ya nchi.













