Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndoa: Inawezekana wanawake nchini Afrika Kusini kuwa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja?
Mwanzoni, Movumbi Ndzalama alikuwa akishangaa sana kuhusu utamaduni wa kuwa na ndoa ya mtu mmoja, akikumbuka alikuwa akiwauliza wazazi wake, kama wanaweza kuwa pamoja katika maisha yao yote.
"Nilihisi kwamba watu walipaswa kuwa pamoja kwa muda fulani," aliiambia BBC.
"Kila kilichonizunguka, kuanzia filamu mpaka kanisani ni kuhusu ndoa ya mume na mke mmoja, lakini sijawahi kuelewa dhana hiyo."
Akiwa na miaka 33 sasa Movumbi anajitambulisha kama mwanamke aliyetokana na kubadilisha jinsia na mwenye mwanaume zaidi ya mmoja, suala linalotoa fursa salama kwa wake wa ndoa moja nchini Afrika Kusini."Kwa sasa nina mwenza wangu mkubwa na nina watoto wake, na mwenza wangu mwingine hana tatizo na hilo, anafurahia," alisema.
Mwanamke kuwa na mume mmoja
Afrika Kusini ina moja ya sheria za kiliberali , zinazoruhusu ndoa za jinsia moja na kuruhusu mitala kwa wanaume. Kwa sasa taifa hilo linafikiria kurekebisha sheria zake za ndoa, na moja ya swali kubwa la msingi linaloibuka hapa, ni kama ndoa za mume wengi zitaruhusiwa, kama mwanamke anaweza kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
Suala hili limekumbana na upinzani mubwa kutoka upande wa wahafidhina.
Mfanyabiashara na mtangazaji maarufu wa televisheni Moussa Mesiliko, mwenye watoto wanne, aliuliza: "Utamaduni huu wa kiafrika ukiondolewa, itakuwaje kuhusu watoto wa watu hawa? Watajitambuaje wao ni kina nani?"
Akaongeza: "wanawake kwa sasa hawawezi kutekeleza majukumu ya wanaume, hatujawahi kusikia hili, mwanaume atalipa mahari kwa mwanaume? Mwanaume atachukua na kutumia jina la mkewe?"
Watu wengine akiwemo mchungaji Kenneth Michaud wa chama cha African Christian Democratic alisema suala hilo "litaiharibu jamii."
"Utafikia muda mmoja wa wanaume hao wawili watamwambia mwanamke wao, "unatumia muda mwingi na mume mwenzangu kuliko mie, hapo kutazuka mgogoro baina ya wanaume hao."
Imani za watu zatikiswa
Movumbi anaelewa kwamba huu ni wakati muhimu kwa wanawake waliokuwepo katika mahusiano ya wanandoa zaidi ya mmoja na anasema, "hali ya sasa ni tete, na imani nyingi za watu zitatikisika."
"Wanaume wamekuw wakioa mwanaume zaidi ya mmoja bila kificho na wamekuwa wakifurahia ndoa hiyo kwa vizazi na vizazi."
Movumbi amejiweka wazi kama mtu aliyejibadilisha jinsia na mtu mwenye ndoa nyingi kama jamii inavyoita - kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Kwa sasa yuko kwenye mahusiano na wanaume wawili, mmoja ambaye ndiye mkubwa amekuwa akiishi naye pamoja na kushirikiana kwa mambo mengi na mwingine ni wa kujifuahisha" ambaye amekuwa akikutana nae mara moja moja na kufurahia mahusiano nae.
"Tumekuwa tukifuata ratiba ya kuwa kwenye mahusiano ya watu wengi, kwa namna tunavyoweza kuwafahamu wenza wa wenzetu, si muhimu sana kupendana, lakini nahitaji uwazi huu ukubalike na liwe jambo la kawaida," anasema.
Awali alikuwa ana wasiwasi wa kuifahamisha familia yake, lakini akaamua kuwasiliana nao miaka mitano iliyopita, wakati uhusiano wake na mwenza ama mume mkubwa Mzu Niamyakila Nelapatsi ulipokuwa umeimarika.
"Mwenza wangu mkubwa na yeye anaaamini katika uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja, na sikutaka famiia yangu imfumanie na mtu mwingine na kuleta kizaazaa," anasema.
"Wakati huo binti yangu alikuwa na miaka mitano na nilianza shughuli hii na kwenda kwenye vituo vye televisheni kuendesha kampeni kuhusu doa za waume zaidi ya mmoja , sikutaka wafahamu kupitia kwingine."
Movumbi anasema kiasi fulani aliungwa mkono, lakini bado safari ni ndefu. Anakumbuka wakati wa sherehe ya mwisho ya uchumba, mwenza wake alisema. "wananiuliza kama kuna mwanaume mwingine anatarajiwa kuja na kulipa hamari, kwa hiyo nikawaambia, hilo linawezekana," anasema.
"Lazima niishi kwenye ukweli, ama wakubaliane nao."
"Mfumo dume kikwazo"
Wanaharaki wa haki za kijinsia kwa sasa wanaendesha kampeni ya kuhalalishwa kwa ndoa za mwanaume zaidi ya mmoja nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuleta uhuru wa kuchagua, ambapo kwa sasa, sheria zinatambua na kuruhusu mwanaume kuaoa mke zaidi ya mmoja.
Wazo na hoja hiyo imeingizwa kwenye nyaraka ya serikali kwa ajili ya mjadala na huenda ukachochea mabadiliko makubwa ya shria za ndoa tangu mwaka 1994.
Nyaraka hiyo inapendekeza pia kutambuliwa kisheria kwa ndoa za kiislamu, Wahindu, Wayahudi na marastafariani, ambazo kwa sasa zinachukuliwa kama batili.
Movumbi anasema wasiwasi ulioibuliwa kuhusu mitala umejikita katika mfumo dume.
Profesa Collis Machoko, mtaalam wa ndoa za mtu zaidi ya mmoja anaona ishara sawa na Movumbi: "uliopokuja ukristo na ukoloni, wajibu wa mwanamke ulipungua, hawakuwa sawa na wanaume, na ndoa zikawa kama moja ya nyenzo zilizotumika kujenga himaya ya utawala."
Utamaduni wa ndoa ya mwenza zaidi ya mmoja ilikua ya kawaida nchini Kenya, DRC na Ngeria, na umeendelea kutekelezwa nchini Gabon, ambapo sheria inaruhusu.
"Suala la watoto ni rahisi, watoto wakizaliwa katika mahusiano ya aina hii lolote likitokea watasalia kuwa watoto wa familia hiyo."
"Vita tofauti na ya kipekee''
Movumbi anasema "wanaume wengi wanasema walikuwa hawana tatizo kuwa sehemu ya mitala," anakumbuka.
"Kuwa katika mahusiano a mtu zaidi ya mmoja sio jambo nalotumia kupata wapenzi wengi nitakavyo, lakini ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye nina hisia nae."
Movumbi alikutana na wanaume wake kupitia kundi la kwenye mtandao wa kijamii linalotaka kuwaleta watu wenye mahusiano ya mtu zaidi ya mmoja pamoja nchini Afrika Kusini.
Wakati huu taifa hilo likiendelea na mjadala wa kutambua aina hiyo ya mahusiano kuwa ya kisheria, Movumbi anasema ameunda jukwaa la mtandao aliloliita "Mapenzi ya wazi Afrika" akishirikiana na mumewe mkubwa.
"Jukwaa hili ni zawadi kwa watu ambao wanaunga mkono ndoa ama mahusiano ya mtu zaidi ya mmoja, natumaini wamepata njia na hawataishi kwa kudanganya. Kama ilivyo kwa vita zingine, watakuwepo watu ambao watapinga hili tunalopigania', anasema na kuongeza "wakati mama yangu akiwa na uja uzito wangu, alikuwa akijifanya kupigania uzazi wa mpango bila ridhaa ya mwanaume."
"Ilikuwa vita tofauti wakati huo, na hii sasa pia ni vita tofauti."