Serikali ya Tanzania yatangaza tahadhari ya mlipuko wa homa ya uti wa mgongo
Iliyochapishwa
Serikali ya Tanzania imetangaza tahadhari ya kiafya kufuatia mlipuko wa homa ya uti wa mgongo uliotokea katika jimbo la Tshopo nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Mganga mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt. Aifelo Sichwale ameiambia BBC kuwa Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo nchini DRC na kuchukua hatua ili kuzuia na kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini kama alivyozungumza na Martha Saranga