Maisha katika nyuzi joto 50: Jinsi ya kupoza jiji kubwa

Maelezo ya video, Maisha katika nyuzi joto 50: Jinsi ya kupoza jiji kubwa
Iliyochapishwa

Mwaka 2021 ukiwa ni moja ya miaka iliyorekodi viwango vya juu vya joto duniani, miji mingine mikubwa inapambana na kuongezeka kwa joto. Hii inaweza kusababisha shida ya kupumua, uchovu na kiharusi cha joto.

Lakini huko Pakistan, wakati wengine wanapambana kuunda hewa iliyopozwa kwa kutumia kiyoyozi, mtu mmoja anajaribu kupata suluhisho kwa kupanda misitu ya mijini.