Korea kaskazini yafyatua makombora 2 ya masafa marefu, yasema Korea Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
Korea Kaaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu kutoka pwani ya mashariki ya taifa hilo , jeshi la Korea Kusini limethibitisha.
Japan pia iliripoti kwamba kuna kitu kilichofyatuliwa kuelekea angani ambacho inahisi huenda ni kombora la masafa mrefu.
Waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga amelitaja jaribio hilo la kombora kama la kikatili akisema linatishia usalama na amani ya eneo hilo.
Ni jaribio la pili la silaha kufanywa wiki hii, huku la kwanza likiwa kombora la masafa mafupi.
Haijulikani ni wapi makombora hayo yalianguka , lakini mkuu mwenza wa majeshi nchini Korea kusini amesema kwamba jeshi la taifa hilo limejiandaa vilivyo likishirikiana kwa karibu na lile la Marekani.
Majaribio ya silaha za masafa marefu yanakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia mipango wa kinyuklia ya taifa la Korea kaskazini.
Silaha hizo zinaweza kubeba vichwa vya kinyuklia na huorodheshwa kulingana na umbali ambao yanaweza kufika - huku kombora linalosafiri umbali zaidi likiwa lile linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine kwa jina (ICBM).
Korea kaskazini awali imefanikiwa kufanyia majaribio kombora la ICBM ambalo linadaiwa kuwa na uwezo wa kufika magharibi mwa Ulaya na nusu ya bara la Marekani.
Siku ya Jumatatu, Korea kaskazini ilifanyia majaribio kombora la masafa mafupi lililodaiwa kuwa na uwezo wa kushambulia eneo kubwa la Japan , likitaja kombora hilo kama lile la kimkakati na lenye umuhimu mkubwa.
Chuo cha taifa cha mafunzo ya sayansi ya mafunzo ilifanya zoezi la jaribio hilo la kombola la masafa marefu Korea Kaskazini kama ilivyochukuliwa katika picha kadhaa ambazo hazina tarehe lakini zilisambazwa na wakala wa habari wa Korea Kaskazini -KCNA tarehe 13 Septemba 2021.

Chanzo cha picha, KCNA
Wataalamu wanasema kombora hilo lina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linasema halikatazi majaribio ya makombora ya masafa marefu lakini inaangalia namna ambavyo makombora hayo yanaweza kuwa hatari zaidi kwa sababu yana uwezo wa kubeba silaha kubwa na zenye nguvu zaidi pamoja na kuwa na nguvu ya kusafiri kwa kasi.
Korea ya kaskazini inakabiliwa na uhaba wa chakula na uchumi kuporomoka - jambo linalozua maswali ni wamewezaje kuweza kutengeza silaha wakati wakiwa katika hali kama hiyo .
Taifa hilo limejitenga kwa zaidi ya mwaka .
Limefunga mahusiano ya kibiashara na hata kutaka mshirika wake China kuacha kusambaza virusi vya corona.Waziri wa mambo ya nje wa China anataka kufanya mazungumzo Korea Kusini huko Seoul siku ya Jumatano.Mpango wa silaha wa Korea Kaskazini na uzalishaji wa nyuklia zinaweza kuwa ajenda.
Mwezi Machi mwaka huu, Korea ya kaskazini ikataa vikwazo vilivyowekewa dhidi ya majaribio ya makombora ya masafa marefu ambapo Marekani , Japan na Korea Kusini ililaani vikali.
Na mwezi uliopita wakala wa Umoja wa Mataifa wa atomiki walisema Korea Kaskazini ilionekana kuanza kutengeneza tena silaha za nuklia, na kuuita kuwa na maendeleo ya kusumbua zaidi.












