Pendo Njau: Mfahamu mwanamke shupavu mwamuzi wa masumbwi Tanzania

Iliyochapishwa

Pendo Njau ni mwamuzi wa masumbwi kinara kwa sasa nchini Tanzania akiwa na rekodi ya kuchezesha mapambano makubwa zaidi nchini Tanzania siku za karibuni

Safari yake katika masumbwi haikuwa rahisi kama mwanamke tangu awali jamii ilimshangaa kwani walio wengi waliamini mchezo huo ni wa wahuni tu

Pendo ambaye ni mama wa watoto wawili aliiambia BBC wazazi wake na familia yake ndio nguzo imara za mafanikio yake