Onesmo Mbasha: Tazama jinsi biashara ya kuuza uume wa ng'ombe inavyomtajirisha Mtanzania huyu
Iliyochapishwa
Onesmo Mbasha ambaye zamani alikuwa mfanyabiashara wa mavazi sasa anajipatia mamilioni ya fedha kwa kuuza uume wa ng'ombe kwa Wachina ambao wao wanadai wanautumia kutengeneza nyuzi za kushonea binadamu.
Anasema awali vitu hivyo havikuwa na soko kwani wachache waliokuwa wakihitaji ilikuwa ni kwa ajili ya supu na dawa kwa maelekezo ya waganga wa kienyeji.
Mwandishi wetu Eagan Salla alimtembelea sokoni kwake vingunguti ambapo pia huuza nyama za mbuzi na ngombe pamoja na vichwa na miguu