Fahamu jinsi Kenya inavyofanya hesabu kubwa zaidi ya wanyama

Iliyochapishwa

Kenya inafanya sensa kubwa ya Wanyama katika historia yake. Wanyama pori wote ardhini na majini wanahesabiwa ili kusaidia katika juhudi za uhifadhi na kufufua utalii.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni nyumbani kwa spishi za wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia wakiwemo simba, twiga na faru wawili wa weupe (Northern White Rhino ) waliosalia duniani.

Pia ni njia ya uhamiaji wa nyangumi ,p na kobe wa baharini wanaokabiliwa na tisho la kuangamia.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi ametuandalia taarifa ifuatayo kutoka Hifadhi za Bahari na Hifadhi za Misitu za Pwani ya Kenya.