Watoto 2000 waliopoteana na familia zao wakati wa mlipuko wa volcano DRC waungana tena na familia
Iliyochapishwa
Miezi kadhaa baada ya volkano kulipuka karibu na mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mashirika ya misaada bado yanajaribu kuwaunganisha watoto waliotengwa na familia zao.
Binti mmja kwa jina Sarah, ambaye hufanya kazi na watoto wa mitaani, ameifanya kazi ya kuwaunganisha watoto na wazazi wao.