'Catch up': Mpango unaowapatia matumaini wasichana walio wacha shule Kenya
Iliyochapishwa
Huku viongozi wakiendelea na mazungumzo jinsi ya kuwapatia elimu watoto kutoka familia masikini duniani, katika mkutano wa Global Education Summit, nchini Kenya programu moja inawapatia matumaini akina mama walio na umri mdogo ambao wamewacha shule. Vituo vya ‘Catch up’ vinawaruhusu wasichana hao kupata fursa ya pili ya elimu ili kuweza kurudi katika masomo ya kawaida ama kuwa wafanyabiashara. Vituo hivyo vinafanya operesheni zao katika kaunti tano nchini Kenya. Mwandishi wa BBC kuhusu masuala ya wanawake Afrika mashariki Esther Ogola alitembelea mojawapo ya vituo hivyo mashariki mwa Kenya.