Jinsi wanawake wa Roma walivyokatwa kizazi bila ridhaa yao

Iliyochapishwa

Elena alikatwa kizazi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kujifungua mara ya pili. Hakujua kilichofanyika lakini iliumwa sana, kiasa cha kuweza kusaini chochote. Inaaminiwa kwamba mamia ya wanawake wengi wao kutoka jamii ya Waroma walio wachache walikawa kizazi bila idhini yao katika iliyokuwa Czechoslovakia miaka ya 1970 na 1980. Hatua ya nchi hiyo kutenganishwa na kuwa Jamhuri ya Czech na Slovakia mwaka 1993 imefany akuwa ngumu kutafuta haki.