Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: 'Nilihisi uchovu tu kwa saa chache baada ya kuchanjwa, sasa niko sawa’
Iliyochapishwa
Wahudumu wa afya visiwani Zanzibar wameanza kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya covid-19.
Serikali ya Zanzibar imethibitisha kuwa dozi za Sinocav kutoka nchini China zimeanza kutolewa kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajiwa kufanyika baada ya wiki mbili kutoka sasa.
Msikilize daktari mmoja aliyechanjwa na mwingine anayetarajiwa kuchanjwa hivi karibuni kama walivyozungumza na mwandishi wetu Martha Saranga.