Maziko Kagera: Wahaya huzikwa karibu na nyumba zao
Iliyochapishwa
Jamii nyingi Barani Afrika huwa na utamaduni maalum wa kuzika ama kuhifadhi wapendwa wao.
Huko kaskazini magharibi mwa Tanzania mtu akifa basi huzikwa karibu na nyumba yake, utaratibu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
Lakini hivi karibuni imetokea vuta nikuvute baina ya serikali na jamii baada ya agizo la kuzika katika makaburi ya umma.
Jambo ambalo limewalazimu baadhi ya wakazi wa wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kuzika hata usiku ili kuenzi mila hiyo.