Chipsi mayai: Kwa nini 'zege' ni chakula maarufu Dar es Salaam?

Iliyochapishwa

Katika mfululizo wa Makala ya chakula cha mtaani eneo la Afrika mashariki, leo tunaangazia chakula cha ‘chips yai.’

Moja ya vitu vilivyotapakaa katika kila kona ya jiji la Dar es Salaam ni vibanda ama migahawa inayouza viazi mbatata vya kukaanga, maarufu kama chipsi. Katika vibanda hivyo, chakula maarufu zaidi ni chipsi mayai ama 'zege'.

Je chakula hicho kinataengenezwa vipi? Ni kitamu kiasi gani? Na je, ni kweli kuwa kinaliwa zaidi na wanawake? Mwandishi wa BBC Munira Hussein ameandaa taarifa hii:

Chakula hiki kimejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania. Wauzaji wanasema kuwa wateja wakubwa ni wanawake kuliko wanaume.

Unadhani kwa nini wanawake hupendelea chakula hiki zaidi?

Video: Munira Hussein