Caitríona Lagan: "Nacheza vyombo vyote katika bendi yangu ya muziki ya Ireland"
Iliyochapishwa
Caitríona Lagan alianza kuweka mtandaoni video zake akicheza ala tano za muziki - banjo, mandolin, fiddle, guitar na mandola – kwa pamoja, wakati wa Lockdown.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka Londonderry, Kaskazini mwa Ireland,alikuwa akitarajia video zake zitawafurahisha watu wakati wa janga la corona na zimepokelewa vizuri.