Nyota maarufu wa mtandao wa TikTok Misri afungwa kwa tuhuma za uuzaji wa binadamu

Chanzo cha picha, hanenhossamofficial1___
Nyota maarufu kwenye mtandao wa TikTok anashikiliwa na mamlaka nchini Misri, ikiwa ni siku mbili baada yeye na mwenzake mwenye ushawishi kwenye mtandao huo kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya kusafirisha binadamu na kuhukumiwakufungo cha muda mrefu.
Haneen Hossam, 20, aliweka kwenye mtandao huo kipande cha video jumatatu akiomba huruma , akisema hajawahi kumdhuru mtu yeyote
Jumapili, Mahakam jijini Cairo, ilimuhukumu Haneem ambaye hakuwepo mahakamani kwenda jela miaka 10 huku mwenzie Mawada al-Adham, 23,ambaye alikuwepo alihukumiwa miaka sita jela.
wanalikuwa wanatuhumiwa kujitpatia fedha kwa kuwatumia mabinti wanaotuma video zao kwewnye mtandao huo.
Hukumu hiyo imekuja baada ya miezi mitano kutengua hukumu waliyopewa Hossam na Adham kwa kkwenda kinyumae na misnig ya familia kutokana na video walizoweka kwenya mtandao wa TikTok.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema wanawake hao wamehukumiwa kwa kile walichokiita ni ukandazaji unaoendelea wa mamlaka nchini humo unaowalenga watumiaji na watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwafungulia mashitaka yanayokiuka haki zao za faragha na uhuru wao wa kujieleza.
Hossam, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Cairo ambaye anawafuasi karibu 900,000 kqwenye mtandao wa TikTok, kwa mara ya kwanz aalikamatwa April 2020 baada ya kuweka kwenye mtandao huo video ikiwaalika wafuasi wake wa kike kujiunga kwenye mtandao mwingine wa video unaoitwa Likee, akiwamabia wanaweza kutengeneza fedha. Badae mwendesha mashitaka akamshitaki kwa kwenda kinyume na misngi ya familia.
Adham, ambaye alikuwa na wafuasi milioni 3 kwenye TikTok na milioni 1.4 kwenye mtandao wa Instagram, alituhumiwa kwa kosa kama la mwenzie, mwezi mmoja baadae.

Chanzo cha picha, AFP
Mwezi Julai, Mhakama ya kiuchumi iliwatia hatiani Hossam na Adham na kuwahukumu kwenda jela miaka miwili.
Hukumu hiyo iliondolewa mwezi January mwaka huu na wakaachiwa mwezi mmopja baadae, hata hivyo mashtaka mpaya ya kusafirisha binadamu yakafuynguliwa dhidi yao.
Watu wengine watatu wamehukumuwa kwenda jela miaka sita kila mmoja kwa kuwasaidia mabinti hao kutekeleza unaotajwa ni uhalifu wa kufanya biashara ya kusafirisha watu.
Wakili wa Hossam, Hani Sameh, alisema mteja wake huyo amehukumiw akifunga cha muda mrefu kwa vile hakuhufdhuria mahakamani.
Hossam amesikitishwa na hukumu hiyo na kumuomba rais Abdul Fattah al-Sisi kumpa msamaha wa rais, ameomba hilo kupitia video aliyoituma kwneye mtandao wake wa Insatagrama muda mfupi kabla hajakamatwa.
'Miaka 10 jela, hata sistahili haya, nilikuwa jela kwa miezi kumi, na sijasema neno lolote nilivyotoka, kwanini mnataka kunifunga tena?, alisema Hossam.














