Tanzania kujiunga na mpango wa chanjo ya corona ya WHO kwa jina Covax
Iliyochapishwa
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limepokea taarifa rasmi ya Tanzania kuomba kujiunga na mpango wa COVAX unaolenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo.
Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt Matshidiso Moeti amesema hii leo kuwa chanjo hizo zinaweza kuingia Tanzania katika kipindi cha wiki mbili.