Temitope Balogun Joshua: Wafuasi wake wasema 'yuko usingizini atarudi'

Maelezo ya sauti, Wafuasi wa SCOAN: 'TB Joshua yuko usingizini atarudi'
Iliyochapishwa

Habari za kifo cha Mhubiri maarufu, Temitope Balogun Joshua, maarufu kwa jina la T.B Joshua zimewashangaza raia wengi wa Nigeria na dunia kwa ujumla.

Kanisa la Sinagogi kwa mataifa yote SCOAN ambalo lilianzishwa na mhubiri huyo lilithibitisha habari za kifo chake Jumapili alfajiri, huku chanzo kikiwa bado hakijawekwa bayana.

Lakini ni kwa namna gani raia nchini humo waliopokea taarifa za kifo hicho? Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amezungumza na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dkt. Benson Bana.