Shimo kubwa la mviringo linalotishia 'kuangamiza nyumba lazua hofu Pueblo, Mexico
Iliyochapishwa
Sauti kubwa ilisikika miongoni mwa wakaazi wa mji wa Puebla , katikati ya Mexico Jumamosi tarehe 29 mwezi Mei.
Kilichowashangaza majirani ni ugunduzi kwamba kipande cha ardhi kilikuwa kikizama.
Kutoka siku hiyo hadi sasa kile kilichoanza kuwa shimo la mviringo wa mita tano kiliendelea kuwa na mviringo wa mita 80 na kina cha mita 20.