Tanzania:Ni vigezo vipi vinavyotumiwa kuamua mtu hajavalia ifaavyo bungeni?
Baadhi ya wabunge wanawake nchini Tanzania wanataka mbunge mwenzao Condester Sichwale aliyetolewa nje ya kikao cha bunge, kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi,aweze kuombwa radhi.
Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai aliamuru mbunge huyo kutolewa nje kutokana na suruali aliyokuwa ameivaa kuonekana kumbana,madai yaliyotolewa na mbunge mwenzake ambaye alitaka kuona sheria ikichukua mkondo wake dhidi ya mbunge Condester.
Katika gumzo ,tunadadisi kwa kina kuhusiana na hatua hiyo ya mbunge huyo kutolewa nje ya bunge sababu ya mavazi yake, Je? kunaleta taswira gani?
Leonard Mubali amezungumza Mbunge Stellah Manyanya kutoka Tanzania, mbunge Zulekha Hassan kutoka Kenya na Nerima Wako, mwanaharakati wa masuala ya mavazi.Kwanza Mbunge Stellah Manyanya, anaeleza kanuni zinasema nini kuhusu mavazi bungeni