Mlipuko wa Volkano DR Congo: Wanawake wajifungua watoto njiti kutokana na mlipuko wa Volka

Iliyochapishwa

Zaidi ya Wanawake mia moja katika mji wa Goma na viungani mwake, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezaa watoto njiti au mimba zao kuharibika, tangu kutokea kwa mlipuko wa volkano katika mlima wa Nyiragongo.

Hayo yanakuja huku takriban watu laki tano mjini humo wakiachwa bila maji safi ya kunywa baada ya mlipuko wa volkano karibu wiki mbili zilizopita.

Muda mfupi uliopita nimezungumza na Daktari Alex Kasanzu akiwa mjini Goma kutupa picha kamili kuhusu hali ya kiafya katika eneo hilo.