Mahakama ya kwenye gari inavyosaidia watu wa hali ya chini Tanzania
Iliyochapishwa
Nchini Tanzania sio jambo la kustaajabisha kesi kuchukua hata zaidi ya mwaka mmoja hadi kutolewa hukumu, lakini kwa kuanzishwa mahakama zinazotembea inategemewa kutatua changamoto hii kwa kupunguza wingi wa mashauri katika mahakama za mwanzo.
Magari hayo yanayotumika kama mahakama yanaenda kutoa huduma ya kimahakama katika maeneo ya vijijini ambapo ni mbali na majengo ya mahakama. Mradi huu umefadhiliwa na Benki ya Dunia kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 65.
Humphrey Mgonja amefuatilia taarifa hiyo kujua uwepo ma mahakama hizo umeleta mabadiliko yoyote?