Mgawanyiko wakumba kanisa katoliki Ujerumani kutokana na haki za wapenzi wa jinsia moja

Iliyochapishwa

Mlio wa Kengele ya kanisani unapungua , na vyombo vya muziki vinaanza kucheza naye Jan Korditschke anaelekea katika madhabahu kuanzisha misa .

Inaonekana kama siku ya kawaida na Ibada ya Jumapili ya kanisa katoliki.

Lakini kuna hisia zisizo za kawaida. Kuna kitu kisicho cha kawaida ambacho kinatarajiwa kufanyika. Fr Korditschke anasema kwamba mtu yeyote ambaye angependelea kupokea baraka asimame.

Idadi kubwa ya waumini waliopo ndani ya kanisa wanasimama, ikiwemo makumi ya wanandoa wa jinsia moja.

Huku muziki ukiendelea kucheza , kuhani anazunguka ndani ya kanisa hilo polepole , huku akiwauliza wale waliosimama ni aina gani ya maombi wangetaka kuombewa.

Baadaye anaiunua mikono yake juu ya vichwa vya watu walioinama na kuwanong'onezea wanachotaka kuombewa.

Wengi wanaonekana wakibubujikwa na machozi . Hii ni kwasababu kwa mara ya kwanza wapenzi wa jinsia moja wamehisi kukubalika ndani ya kanisa hilo.

''Ni uchungu sana na nimebaini jinsi nilivyojeruhiwa'', anasema Sangha, ambaye ameishi maisha yake yote kama mkatoliki , aliye na Frieda mpenzi wake kwa zaidi ya miaka 25.

''Kwa miaka 49 sijakaribishwa. Lakini hatimaye watu wanaanza kusema kwamba : Ni sawa kwamba uko hapa''.

.Jinsi Vatican ilivyowashangaza Wapenzi wa jinsi moja

Kwa Matthias, ambaye alizaliwa mkatoliki alipokea baraka na mpenzi wake Thomas , na kwamba kuhudhuria ibada ya Misa halijawa tatizo kwao. Lakini taarifa kutoka kwa maafisa Wakatoliki zimemfanya kufikiria kuliwacha kanisa hilo.

''Nimekuwa nikifikiria iwapo nisalie katika kanisa lisilonitaka . lakini kanisa katoliki hapa mashinani linanipatia imani'' .

Cha kushangaza ni kwamba ni taarifa kama hiyo ambayo ilipelekea kufanyika kwa ibada ya leo.

Mnaamo mwezi Machi , Vatican ilitoa taarifa yenye onyo kali , ikizitaja ndoa za wapenzi wa jinsia moja kuwa 'dhambi' na kusisitiza kuwapiga marufuku wahubiri wanaobariki ndoa hizo.

Hiki ni kitu cha kibinafsi ambacho Wahubiri wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wamekuwa wakifanya - lakini hadi kufikia sasa sio hadharani.

Pastoral worker Brigitte Schmidt blesses the same-sex couple Nini and Juliana Weinmeister during a ceremony in a Catholic church in Cologne, Germany, May 10, 2021.

Badala yake maelfu ya makuhani, watawa, na waumini walizindua kampeni kwa jina Liebe gwinnt{ Mpenzi hushinda}, ili kuweka wazi hadharani kwamba wapenzi wa jinsia moja wanakaribishwa katika kanisa hilo.

"Nilikasirika na kusikia aibu , kwasababu nahisi ilikuwa taarifa ilioumiza'' , Fr Korditschke aliniambia.

Ni mmoja wa makuhani 120 nchini Ujerumani ambao waliamua hadharani kukiuka marufuku hiyo ya Vatican

Kwanini huwezi kumbariki mtu anayeomboleza?

Katika kipindi cha juma moja wahubiri hao walifanya ibada katika makanisa katoliki kote Ujerumani wakitoa baraka za kibinafsi kwa yeyote aliyewataka , ikiwemo wanandoa ambao kanisa katoliki inawachukulia kama wenye dhambi , kama vile watu waliotalakiana au wapenzi wa jinsia moja.

Nilipomuuliza Fr Korditschke , jinsi alivyo na haki ya kukaidi uamuzi wa Vatican , alijibu kwa machozi machoni.

Kulikuwa na mtu katika kongamano lake ambaye alikuwa ameweka uwa katika kiti chake kwa mpenzi wake aliyefariki miezi michache iliopita , kabla ya kuzungumzia kuhusu uchungu aliokuwa nao na kumuombea baraka ili kumwezesha kukabiliana na tukio hilo.

Kubarikiwa kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja ni mojawapo ya vuguvugu nchini Ujerumani ambapo waumini wa kanisa katoliki wanataka mabadiliko.

Wanawake katika mimbari

Mashirika ya mashinani kama vile Maria 2.0 pia yanapigania haki sawa za wanawake katika kanisa.

Siku moja baada ya ibada ya Fr Korditschke mjini Berlin , wanawake walihubiri kutoka katika mimbari kutoka katika makanisa 12 tofauti nchini Ujerumani kitu ambacho The Vatican pia haikifurahikii.

''Kanisa hilo lilikuwa likisema kwamba dunia ni tambarare na kutuambia ni sharti tuamini hivyo. Kanisa hilo lililazimika kubadili msimamo wake . Ama ulilazimika kuamini kwamba Adam na Eve walikuwa watu wa kawaida'' , anasema Ulrike Goken Huismann, ambaye alitoa hutuba kanisani mjini Dusseldorf.

Sio kwamba kanisa halitabadili mafunzo yake.

Uongozi wa kanisa hilo la Ujerumani umagawanyika : Upande mmoja Maaskofu wanaomba kuwepo kwa mabadiliko huku wengine wakiunga mkono msimamo mkali wa Vatican.

Hatahivyo, utafiti unasema kwamba Wakatoliki binafsi nchini Ujerumani wana msimamo wa kadri zaidi ya Uongozi wa kanisa hilo.

Utafiti mmoja , uliofanywa na Chuo kikuu cha Berlin na Munster unasema kwamba asilimia 70 ya Wakatoliki Wajerumani wanaunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja, huku asilimia 80 wakiwa hawana tatizo na wanandoa wanaoishi pamoja nje ya ndoa na asilimia 85 wanaamini kwamba wahubiri wanapaswa kuruhusiwa kufunga ndoa.

Baada ya baraka za wapenzi wa jinsia moja kutolewa mjini Berlin, takriban watu 100 wanakongamana nje ya kanisa kunywa kikombe cha mvinyo na kusherehekea katika jua.

Lakini katika lango la kanisa hilo , kuna takriban waandamanaji 10 wanaosema kwamba ''Mungu habariki dhambi''.

Hakuna uadui kati ya makundi hayo mawili, lakini yote yanapaza sauti yakiwa na maono tofauti.

Hiyo pia ni sawa anasema Fr Korditschke akitabasamu.

Kile ambacho Papa amesema kuhusu wapenzi wa jinsia moja

Oktoba 2020: Papa Francis alisema kwamba wapenzi wa jinsia moja wanapaswa kuruhusiwa kuoana. ''Wapenzi wa jinsia moja ni Watoto wa Mungu na wana haki kuwa na familia. Hakuna mtu anapaswa kufukuzwa ama kuakandamizwa kwasababu."

Oktoba 2014: Maaskofu katika uongozi wa kanisa hilo wawasilisha maombi ya kuwakubali wapenzi wa jinsia moja ambao waliungwa mkono na papa .

Julai 2013: Akiwa katika ndege Papa awaambia maripota kwamba hawafai kukandamizwa na badala yake wanapaswa kukubalika katika jamii.

''Viongozi wa dini walio wapenzi wa jinsia moja wanapaswa kusamehewa na dhambi zao kusahaulika''a, alisema.

2013: Katika kitabu cha mbinguni , Papa anasema kwamba kulinganishwa kisheria kwa mahusiano ya jinsia moja na ndoa za kawaida ni ukandamizaji wa tabia za wanadamu ".

2010: Kama Askofu wa Buenos Aires apinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja lakini aunga mkono kulindwa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja.