Ghasia za siku ya Idd RDC : Mahakama yawahukumu kifo watu 29

People inspect a burned police car, after two groups of Muslims clashed outside Martyrs' Stadium in Kinshasa, Democratic Republic of Congo - 13 May 2021

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, gari la polisi pia liliharibiwa katika makabiliano hayo nje ya uwanja wa Mashahidi
Iliyochapishwa

Watu ishirini na tisa wamehukumiwa kifo katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kutokana na ghasia za siku ya Idd al Fitr zilizoibuka katika mji mkuu Kinshasa.

Afisa mmoja wa polisi ialiuawa na makumi kadhaa ya watu wengine walijeruhiwa katika makabiliano baina ya makundi mawili hasimu ya kiislamu.

Walikuwa wamekusanyika kusherehekea kilele cha mfungo wa mwezi wa Ramadhan, lakini hawakuelewana juu ya ni nani anayepaswa kuongoza tukio la sherehe hizo, ikiwemo ibada.

Hukumu hiyo haitekelezwi tena katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na badala yake wale wanaohukumiwa kifo hutumikia kifungo maisha yao yote yaliyosalia.

Kesi ilitangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari

Polisi walitumia gesi za kutoa machozi na risasi za plastiki kuwatanya maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya wanja mjini Kinshasa siku ya Alhamisi kwa ajili ya sherehe za Idd al-Fitr.

Polisi kadhaa waliumia katika ghasia hizo na bado wako mahututi, wanasema maafisa.

A wounded policeman, Nsonso Lenga Lambert, sits in a police vehicle that was damaged when two groups of Muslims clashed outside Martyrs' Stadium in Kinshasa, Democratic Republic of Congo - 13 May 2021.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, mmoja wa maafisa wa polisi aliyejeruhiwa katika makabiliano ya siku ya Idd alipigwa picha ndani ya gari nje ya uwanja siku ya alhamisi

Makabiliano hayo yalichochewa na mzozo baina ya kambi mbili za Waislamu.

Watu arobaini na mmoja walikamatwa katika eneo la tukio na kesi yao iliendeshwa Ijumaa.

Tukio la kesi hiyo lilionyeshwa moja kwa moja kupitia kwenye televisheni na kuendelea usiku kucha.

Muslim at Eid prayers at the Martyrs' Stadium in Kinshasa, DR Congo - June 201

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kwa kawaida ibada za Idd al-Fitr hufanyika kwa amani - na hii ni picha ya waumini wa kiislamu wakiswali siku ya Idd katika uwanja wa Mashahidi -Martyrs' Stadium mwaka 2017

Watu 31 nchio waliopatikana na hatia - watu 29 wakahukumiwa kifo huku wawili wakihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Kutokana na namna hukumu ilivyotolewa haraka kutakuwa na uwezekano wa kutokea kwa hofu juu ya haki katika kesi hiyo, anasema mhariri wa BBC wa masuala ya Afrika Will Ross.