Pacha wake Joseph Kabila ataka tuhuma dhidi ya familia yao zipuuziwe

Iliyochapishwa

Familia ya aliyekuwa rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila inashutumiwa kufadhili makundi ya waasi hasa viongozi wa jadi katika jimbo la Tanganyika kwa lengo la kumuondoa madarakani rais wa sasa Felix Tshishekedi.

Pia kuna madai kwamba familia hiyo ya Rais Mstaafu Kabila inafadhili makundi ya wanasiasa na wanaharakati ili kuipinga serikali iliyopo madarakani.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na Mwandishi wetu Mbelechi Msoshi Bi.Jeannette Kabila ambaye ni dada yake Rais Mstaafu Joseph Kabila amekanusha tuhuma hizo.