Dawa za kutengeneza mwili wenye 'Umbo namba nane' zilivyohatarisha maisha ya wanawake
Iliyochapishwa
Kwa Altou mwanamitindo wa miaka 19 anaamini mwili wa 'umbo namba nane' ni muhimu katika kupata 'likes' na kazi zaidi.
Ni mmoja kati ya wanawake maelfu duniani ambao wametumia dawa ya Apetamin, dawa inayotangazwa kwenye mitandao ya kijamii kama dawa ya kujenga mwili kuwa 'umbo namba nane' kama maumbo ya watu maarufu kama vile Kim Kardashian.
Dawa hii inapatikana kwa kiasi kikubwa. Lakini wengi hawajajua kuwa Apetamin ni dawa isiyo na idhini ya matumizi-na matumizi yake mabaya yanasababisha athari kubwa.