Tanzania,Uganda kuwa washirika wakuu wa biashara ya mafuta

Iliyochapishwa

Tanzania na Uganda watakuwa washirika wakuu wa biashara ya mafuta kutokana na ujenzi wa mafuta.

Serikali hizo zimekubaliana katika masuala ya hisa, usafirishaji na ushuru katika hatua za awali za mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi wa jumla ya Kilometa 1,443 kutoka Magharibi mwa Uganda mpaka kwenye bandari ya bahari ya Hindi, Tanga.