Mkoa wa katavi Tanzania waanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama ya wanyamapori

Iliyochapishwa

Mkoa wa Katavi kusini Magharibi mwa Tanzania , umeanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama pori, biashara ambayo ambayo ni adimu katika maeneo yaliyo mengi nchini Tanzania na ukanda wa Afrika. Mkoa huo unahifadhi ya taifa iliyobeka jina la mkoa yaani Katavi,ambamo kuna wanyama pori aina mbali mbali.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera, amezungumza na mwandishi wa BBC Leonard Mubali ambaye ametaka kujua ni utaratibu gani wanaotumia kuwapata wanyama hao ili nyama zao ziweze kuuzwa katika bucha hiyo iliyofunguliwa...