Safari ya maisha ya Mwanamfalme Philip
Iliyochapishwa
Mwanamfalme Philip wa Edinburg na mume wa Malkia mtawala wa Uingereza Malkia Elizabeth wa pili, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Wenza hao wa kifalme walioana zaidi ya miaka 70 iliyopita, baada ya kula viapo vyao tarehe 20 mwezi Novemba mwaka 1947 katika kanisa la Westminster Abbey. Luteni Philip Mountbatten alikuwa na miaka 26 wakati huo, na pia binti mfalme Elizabeth alikuwa na miaka 21. Prince Philip hakuwa kwenye orodha ya kiti cha utawala wa Uingereza, ambacho mtoto wake wa kwanza wa kiume Prince Charles ni mrithi.
Akiwa na nguvu na mtekelezaji kwa vitendo, Prince Philip alisaidia familia ya kifalme ya Uingereza, na anaacha urithi ulipambwa kwa moyo wake wa kujitolea na shughuli za michezo.