Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusu mahindi yake kupigwa marufuku Kenya

Iliyochapishwa

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Profesa Kitila Mkumbo amesema kwamba tamko la kuzuia mahindi yake kuingia nchini Kenya halikufanywa na serikali ya Kenya bali taasisi ambayo hata hivyo majibu yake hayakuwa sahihi.

Katika mahojiano na BBC, Bw. Mkumbo amesema majadiliano baina ya pande mbili yanaendelea ili biashara hiyo kubwa kati ya nchi hizo mbili irejee kama awali.