Kuapishwa kwa Samia Suluhu: Huu sio wakati wa kutazama mbele kwa mashaka

Iliyochapishwa

Rais mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema huu ni wakati wa kutanzama mbele kwa matumaini na kujenga Tanzania moja ambayo Rais Magufuli aliitamani.

Rais Suluhu ameyasema hayo katika hoptuba yake ya kuapishwa rasmi kama Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati Dkt John Pombe Magufuli.