Kifo cha Rais Magufuli: Kuna mambo mazuri aliyoyafanya Magufuli na mambo ambayo hayafurahishi, Zitto

Maelezo ya video, Zitto Kabwe: Kuna mambo mazuri Magufuli aliyoyafanya na mambo kadhaa ambayo hayafurahishi
Iliyochapishwa

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe asema, huu sio wakati wa kukumbuka ni yapi aliyoyafanya Hayati Rais Magufuli na muda wa kujadili tutamkubukaje utafika. Katika mazungumzo na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus jijini Dar es salaam Bw Zitto ameanza kwa kutoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Rais Dkt John Pombe Magufuli.