Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jaji Warioba: Samia Suluhu ataonyesha kwa mfano wanawake wanaweza kuwa viongozi
Iliyochapishwa
Jaji mkuu mstaafu mzee Joseph Sinde Warioba ameiambia BBC kuwa ana imani na Mama Samia na hana shaka lolote juu ya namna mabadiliko ya utawala yatakavyofanyika kwani katiba ya Tanzania iko wazi na itafuatwa.
Katika mazungumzo na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Zuhura Yunus aalianza kwa kumuuliza ni vipi ameupokea msiba wa rais Magufuli?