Kifo cha Rais John Magufuli: Je, Mama Samia anatakiwa kuapishwa lini kuwa rais Tanzania?
Iliyochapishwa
Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.
Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Lakini je, ataapishwa lini kushika wadhifa huo? Mwanasheria Fulgence Massawe ameongea na mwandishi wa BBC Regina Mziwanda juu ya hilo.