Kim Yo-jong: Dada yake Kim Jong-un aitaka Marekani isilete 'mtafaruku'

Kim Jong-un and sister Kim Yo-jong attend the Inter-Korean Summit at the Peace House on April 27, 2018 in Panmunjom, South Korea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kim Yo-jong anatajwa kuwa mshirika mwenye nguvu wa kaka yake Kim Jong-un
Iliyochapishwa

Dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameionya Marekani kutosababisha mtafaruku, wakati Rais Joe Biden akiandaa sera zake kwa Wakorea.

Alinukuliwa kwenye chombo cha habari cha taifa kuwa Kim Yo-jong aliikosoa Marekani na Korea Kusini kwa kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja.

Maoni yake yalikuja siku moja baada ya maofisa wa juu wa Marekani kuwasili Seoul.

Serikali ya Marekani imesema kuwa imekuwa ikijaribu kwa wiki kadhaa kupata mawasiliano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini bado haijamtambua kuwa rais Biden ndio yuko madarakani.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakivutana kuhusu mpango wa nyuklia na ule wa utengenezaji wa mabomu wa Korea Kaskazini

Kim Yo-jong alinukuliwa na na gazeti la Rodong Sinmun akisema : "Neno la ushauri kwa utawala mpya wa Marekani ni kuwa wasihangaike kusambaza unga wa risasi katika eneo letu la bahari.

"Kama wanataka kulala kwa amani kwa miaka minne ijayo , ni vyema kutosababisha mtafaruku wowote katika hatua za mwanzo."

Alilisitiza kwa kusema kuwa taifa lake linapinga mazoezi hayo ya pamoja kwa kuwa wanaamini kuwa hiyo ni njia tu ya kujiandaa kuwavamia "Serikali ya Korea Kusini bado haijachagua vita ya Machi au mgogoro wa Machi.

Donald Trump and North Korea's leader Kim Jong-un talk before a meeting in the Demilitarized Zone (DMZ) on June 30, 2019, in Panmunjom, Korea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mikutano ya Donald Trump na Kim Jong-un ilishindwa kuleta diplomasia

Kim Yo-jong ni mdogo wake Kim Jong-un na ndugu yake pekee ambaye anatajwa kuwa mshirika wake mkuu.

Watu wengi wa Korea Kusini walikuwa wanatarajia haya.

Korea Kaskazini mara nyingi huwa wanaijibu Korea Kusini inapofanya mazoezi ya kijeshi kwa kushirikiana na Marekani.

Mara nyingine huwa ni hata kwa jaribio la kombora. Na mara nyingine huwa inajibu kwa kusema 'michezo wa vita' wakieleza kwa maneno ya hasira.

Kim Yo-jong amekuwa akimwakilisha kaka yake kwa kutoa mashambulio ya namna hiyo hivyo hatua hii si jambo jipya.

Ujumbe wake umelenga kuangalizia mazoezi ya pamoja na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na mkuu wa Ulinzi wa Marekani nchini Korea Kusini.

Huku Marekani na Korea Kusini wakiwa wanafahamu kuwa Korea Kaskazini inaangalia na kusikiliza licha ya ya kutojibu majaribio yoyote ya hivi karibuni yaliyofanywa na Marekani.

Kim Yo-jong hakufafanua kile ambacho Korea Kaskazini inaweza kukifanya kama haikupendezwa na kile walichokisikia katika mkutano. Lakini alisema ameonywa.

line

Mpango Nyuklia wa Korea Kaskazini unatarajiwa kuwa mkubwa katika agenda ya ziara ya wiki hii ya Korea Kusini na Japan na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken pamoja na mkuu wa ulinzi Lloyd Austin.

Bwana Biden ametangaza tayari kuangazia tena sera ya Korea Kaskazini , ambayo anatarajia kuitoa mwezi ujao.

Wakati wa kampeni alimuita bwana Kim "kuwa mualifu na alisema Korea Kaskazini inapaswa kunyang'anywa kabla ya Marekani na Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vya kiuchumi.

Mahusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yalivurugika mwaka 2017, wakati ambapo Korea Kaskazini ilipofanya jaribio la kombora la mali na kupiga maeneo ya Marekani.

Mvutano huo ulipungua wakati rais Donald Trump alipotaka kuweka mahusiano binafsi na bwana Kim.

Lakini pamoja na kuwa na mikutano mingi ukiwemo ule wa Singapore na Vietnam - bado walishindwa kufikia makubailiano kuhusu mpango wa Nyuklia.

line