Yemen:Mvulana asiyeona anayefundisha watoto wenzake katika shule iliyoko eneo la mapigano
Iliyochapishwa
Katika jiji la Taiz, Yemen, mamia ya watoto huhudhuria masomo kila siku katika shule iliyoharibiwa karibu na eneo la mapiganobaina ya serikali na waasi wa Kihudhi .
Ahmed, mvulana mwenye umri wa miaka tisa amabaye amezaliwa na ulemavu wa kutoona , huingilia kati kufundisha wakati waalimo wasipoweza kufanya hivyo. Shule moja kati ya kial shule tano nchini Yemen hazitumiki, kulingana na Unicef. Lakini katika shule hii, waalimu waliamua kufungua masomo , licha ya shule kuharibika, ili elimu iweze kuendelea kutolewa.